00:00
03:36
"Mtaalam" ni wimbo maarufu wa Mbosso, msanii maarufu kutoka Tanzania. Wimbo huu umevutiwa na mashabiki kwa mchanganyiko wake wa R&B na Afropop, pamoja na sauti yake laini na maneno yenye hisia. Mbosso amejidhihirisha katika tasnia ya muziki wa kisasa kutokana na ubunifu wake na uwezo wa kuunganisha mitindo tofauti, jambo ambalo limeimarisha umaarufu wake katika bara la Afrika Mashariki na duniani kote.
Na Mbosso Khan tena
♪
(Sounds by Abbah)
Una kila sababu
Ya kusimama kimaso maso
Mungu kweli wa ajabu
Kanionyesha kwa yangu macho
Chukua zangu swahabu
Mi nibaki na dhambi zako
Unishikishe adabu
Mida ya kulala nitokwe jasho
Mi sijui kupigna mwili wangu wa mapensi dear
♪
Tusipende kugombana mi mwepesi kulialia
Si kujibanabana, raha ya penzi kujiachia
♪
Wako mahututi mama, nimekufa nimejifia
Eeeh! Nalambishwa asali
♪
Kwenye mzinga wa nyuki, tamu ni hatari
♪
Nalambishwa asali
Nachezeshwa buzuki, dudu chalichali
Nimempata!
Nimempata mtaalam nimempata
Nimempata mtaalam nimempata
Nimempata mtaalamu nimempata
Nimempata mtaalamu nimempata
♪
Mi mTanzania wa halali, ila chembechembe za India
Mungu kaninyima ufahari, ila kwa huba najisifia
Sitakuhonga magari, ila mahaba utasanzia
Penzi kachumbari kwa ugali na pilipili ya kushagia
♪
Aah eeh! Nikuite nani?
Majina yote nishamaliza
Aah eeh! Wangu wa ubani
Umeweza kunituliza
Aah eeh! Mambo ya chumbani
Yaani nalala huku napulizwa
Aah eeh! Penzi zito tani
Napewa raha kupitiliza
Eeeh! Nalambishwa asali
Kwenye mzinga wa nyuki, tamu ni hatari
♪
Nalambishwa asali
Nachezeshwa buzuki, dudu chalichali
Nimempata! Nimempata mtaalam nimempata
Nimempata! Nimempata mtaalam nimempata
♪
Mtaalamu wa mapenzi
Nimempata mtaalamu nimempata
Fundi wa mafundi kungwi
Nimempata mtaalamu nimempata
♪
(Kwa Mix Lizer)
♪
Wasafi