00:00
03:30
"Unanionea" ni wimbo maarufu kutoka kwa msanii maarufu wa Bongo Flava, Marioo. Nyimbo hii imepata umaarufu mkubwa katika Afrika Mashariki kutokana na muziki wake unaovutia na maneno ya kina yanayohusu upendo na mahusiano. Marioo ameonyesha ubunifu wake katika kuunganisha melodi za kisasa na ladha za mitindo ya muziki ya kipekee, jambo lililomfanya awe mmoja wa wasanii watakaowapenda na kuwamini mashabiki wake. "Unanionea" imekuwa ikipendwa na kutokea kwenye orodha za nyimbo zilizopendwa na kusisimua katika matukio mbalimbali ya muziki.
Hivi kweli yupo
Mwenye roho mbaya kukushinda
Maana mi sijaona Duniani
♪
Hivi kweli yupo
Aso na haya kukushinda
Maana mie sijaona sijaona
We mtu gani uko radhi
Mwenzako ateketee
Wakati unajua dawa yake
Ni kumponya, nihurumie
Ama mtu gani aliefika
Akaongeza makeke
Na wakati anajua
Mi kwako ndo napona, we nihurumie
Mi najua mapenzi
Sio kwichi kwichi tu
Yanayonogaga mazoea
Nimekuzoea mmmh
Unanionea, mwenzako siwezi matukio mazito
Unanionea, unanipiga mie
Unanionea, unafanya niamini mapenzi mabaya
Unanionea, lalalaa mmmmh
♪
Na kama kuachana nakubali
Sawa fanya yako
Ila sio lazima unionyeshe uniumize
Au kisa unajua
♪
Unaniacha bado nakuhitaji
Ndo unaona bora unikomeshe
Unilize eeeh
Ah poa poa, nishajua vya utamu
Vinakuwaga vya uchungu
Ili doa doa milima haikutani
Japo najua mapenzi
Sio kwichi kwichi tu
Yanayonogaga mazoea
Nimekuzoea mmmh
Unanionea, mwenzako siwezi matukio mazito
Unanionea, unanipiga mie
Unanionea, unafanya niamini mapenzi mabaya
Unanionea, lalalaa
♪
Unanionea, unanionea bure
♪
Hata Bonga anajua unanionea
Chino anajua, unanionea