Nitaubeba - Harmonize

Nitaubeba

Harmonize

00:00

04:10

Song Introduction

"Nitaubeba" ni moja ya nyimbo maarufu za Harmonize, msanii maarufu kutoka Tanzania. Imetolewa mwaka 2016 na imepokea mapenzi mengi kutoka kwa mashabiki wa muziki wa Bongo Flava. Wimbo huu unaonyesha umahiri wa Harmonize katika kubadilisha midundo ya kisasa na maneno yanayovutia. "Nitaubeba" imepata mafanikio makubwa katika orodha za muziki wa Afrika Mashariki na imesaidia kuimarisha umaarufu wa Harmonize katika tasnia ya muziki.

Similar recommendations

Lyric

Imagine uko jangwani umepotea

Mchana juani unatembea

Utokapo ni mbali uendapo ni mbali

Mara ngamia mbebaji akatokea

Na kukushusha mzigo uliokuelemea

Upate afadhali pole na safari

And thats why today

To me yote tisa ila kumi

Umeonesha maana ya upendo

Si kwa maneno bali kwa vitendo

Umeridhika na nilichonacho

Vya watu hutoleagi macho

Siku nikiwa sina twalala

Oooh baby twalala

Aaaah baby if I close my eyes

Mi namuomba Mungu akulinde

Na akusimamie we ndo

Pacha wangu mie

Eti siku hizi vipi mbona sikusikii tena

Sikusikii ukilia sikusikii ukisema

Niko busy na boo jamani nimeshasema

Niko busy na baby na msalaba wake

Nitaubeba, nitaubeba nitaubeba

Na ntafika nao kiume

Nitaubeba (iwe kwenye shida na raha)

Nitaubeba (ama kwenye shibe na njaa)

La kwako ndo langu my darling

Na ntafika nao kiume

Imagine hujifahamu

Umezimia umewekewa damu zinaingia

Bomba ikafunguka na huwezi hata nyanyuka

Mara dakitari wa zamu

Akaingia umepata fahamu unamwangalia

Machozi yanakuanguka unatamani funguka

And that's why today to me

Yote tisa ila kumi unanifurahisha

Kwenye tendo

Au unipe penzi la magendo

Aaaah baby if I close my eyes

Mi namuomba Mungu akulinde

Na akusimamie we ndo pacha wangu mie

Eti siku hizi vipi mbona sikusikii tena

Sikusikii ukilia sikusikii ukisema

Niko busy na boo jamani nimeshasema

Niko busy na baby na msalaba wake

Nitaubeba, nitaubeba nitaubeba

Na ntafika nao kiume

Nitaubeba (iwe kwenye shida na raha)

Ntaubeba (ama kwenye shibe na njaa)

La kwako ndo langu my darling

Na ntafika nao kiume

Iwe kwenye shida na raha

Ama kwenye shibe na njaa

La kwako ndo langu my darling

- It's already the end -