Nitadumu Nae - Yammi

Nitadumu Nae

Yammi

00:00

03:33

Similar recommendations

Lyric

(Aa-ah, ah-ah)

Yammi, Yammi

(Oh, taabani)

(Mafeeling make it)

(Ah-ah)

Ah, ka' kasoma VETA, ye' ni fundi wa mambo

Atwanga pepeta kwa vya juu viwango

Oh, raha naseleleka (selele) mahaba hayaishi bando

Chumba ni hekaheka vita ya unyago na jando

Oh-oh, yeye ndo amenilemaza kulala kwake kifuani

Kutwa kunijaza jaza mi' Kajol yeye Sha Rukh Khan

Anipa mpaka nasaza sebuleni na chumbani

Raha zimenipumbaza mie hoi taabani

Magharibi natafuta sababu

Bibi namtafuta babu

Aniita Ya Qalbi majina ya Kiarabu

Twawachoma mahasidi kwa vinyimbo vya taarabu

Nitadumu nae kwa nguvu za manani

Jaribuni baadae kwa sasa hapatikani

Nitadumu nae kwa nguvu za manani

Jaribuni baadae kwa sasa hapatikani

(Oh-oh), oh-oh (la-la-la), la-la-la (ah-ah), ah-ah

So dawa za China si mizizi ya Congo (ya Congo)

Nampa mchai chai na supu ya kamongo (kamongo)

Oh, full stamina anibeba kwa mugongo (mugongo)

Mambo ya kwenye mtima sio kupendana kwa hongo (kwa hongo)

Oh-oh, yeye ndo amenilemaza kulala kwake kifuani

Kutwa kunijaza jaza mi' Kajol yeye Sha Rukh Khan

Anipa mpaka nasaza sebuleni na chumbani

Kwa raha zimenipumbaza mie hoi taabani

Magharibi natafuta sababu, oh-oh

Bibi namtafuta babu

Aniita Ya Qalbi majina ya Kiarabu

Twawachoma mahasidi kwa vinyimbo vya taarabu

Nitadumu nae kwa nguvu za manani (nguvu za manani, nguvu)

Jaribuni baadae (oh-oh), kwa sasa hapatikani (nimemuweka ndani)

Poleni miungu watu mahodari wa kutabiri (nitadumu nae kwa nguvu za manani)

Hatuachani katu roho zimeungana na miili (jaribuni baadae kwa sasa hapatikani)

Anatembea na roho yangu, anatembea na mwili wangu

Anatembea na pumzi zangu, mimi, mimi, mimi

Kamix Lizer

- It's already the end -