00:00
03:54
"Ukimuona" ni wimbo maarufu wa msanii wa Tanzania, Diamond Platnumz. Wimbo huu unachanganya midundo ya kisasa na maneno ya kuvutia yanayohusu upendo na uhusiano. Baada ya kutolewa, "Ukimuona" imevutia wengi kwa sauti yake ya kipekee na uandishi mzuri, ikiimarisha umaarufu wa Diamond Platnumz katika muziki wa Kiafrika na ulimwengu. Wimbo huu pia umepelekea maonyesho mengi na kushirikiana na wasanii wengine, na kuonyesha uwezo wa Diamond Platnumz kuleta mabadiliko katika tasnia ya muziki.
Mhh mhh
Mungu aliumba Dunia mapenzi tangu tangu
Yashanipiga sasa sinabudi nielewe
Siwezi kung'ang'ania huenda sio fungu langu
Japo ni shida ila nitabaki mwenyewe
Oh, ila mpe shukrani kwa kuniumiza Suraya
Mwambie mi bado maututi, nauguza kidonda changu
Na asisikie hasirani, mwambie mapenzi mabaya
Hata angali hai Khairuki asingetibu gonjwa langu
Kutwa nzima moyo unanidunda dunda (dunda)
Sina amani nasanga rumba (rumba)
Unanidunda dunda
Sema chine tembee moyo oh
Unanidunda dunda (mami moyo)
Sina amani nnasaga rumba (mimi)
Unanidunda dunda
Ehh ukimwona
Ukimwona, ukimwona
♪
Ukimwona, ukimwona
♪
Ukimwona
♪
Nenda mwambie marafiki, marafiki wabaya
Tena wengi waongo wala wasimdanganye
Oya ni mashoga, rafiki; marafiki wabaya ohh mhh
♪
Tatizo mi bado, nilipoteleza nikakosa sipajui
Mpaka akafunga virago na akaamua kuondoka sitambui
Ubaya kinachoniumiza maneno neno maneno oh
Mara kwa ndugu rafiki kwanini anawapa misemo oh
Najaribu papasa labda kwa macho hataona chochote
Ila ndo kutwa mikasa na nnazidi kuanguka niokote
Kutwa nzima moyo unanidunda dunda (dunda)
Sina amani nasanga rumba (rumba)
Unanidunda dunda
Sema chine tembee moyo oh
Unanidunda dunda (mami moyo)
Sina amani nnasaga rumba (oh mimi)
Unanidunda dunda
Ehh ukimwona
Ukimwona, ukimwona
♪
Ukimwona, ukimwona
♪
Ukimwona